Luke 17:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
La! Atamwambia: ‘Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na kunywa.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, badala yake, hatamwambia, ‘Niandalie chakula, nile, jifunge unitumikie ninapokula na kunywa; baadaye unaweza kula na kunywa’?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapana! Utamwambia mtumishi wako, ‘Nitayarishie chakula nile. Jitayarishe na unihudumie. Nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo utakula.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
La! Atamwambia: Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
La! Atamwambia: ‘Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na kunywa.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, badala yake, hatamwambia, ‘Niandalie chakula, nile, jifunge unitumikie ninapokula na kunywa, baadaye waweza kula na kunywa?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, badala yake, hatamwambia, ‘Niandalie chakula, nile, jifunge unitumikie ninapokula na kunywa; baadaye waweza kula na kunywa?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hatamwambia, Nitayarishie chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
La! Atamwambia: ‘Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na kunywa.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hatamwambia: Andalia chakula, nitakachokila, ujifunge nguo, unitumikie, mpaka nitakapokwisha kula na kunywa! Kisha nawe ule, unywe?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Si vile, yeye atamwambia kwanza amupigie chakula na kujitayarisha vizuri kusudi amushugulikie mpaka atakapomaliza kula na kunywa. Kisha pale, ataweza kula na kunywa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
La! kinyume cha hayo, atamwambia, Pakua chakula, nile; jifunge, unikhudumie hatta nikiisha kula na kunywa; na baada ya haya utakula na kunywa mwenyewe.