Luke 18:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: ‘Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: Walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtozaushuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule Farisayo, akasimama, akasali hivi na kuomba kwake mwenyewe: ‘Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang’anyi, wadhalimu, na wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Farisayo alisimama peke yake mbali na mtoza ushuru. Farisayo aliomba akisema, ‘Ee Mungu, ninakushukuru kwa kuwa mimi si mwovu kama watu wengine. Mimi siyo kama wezi, waongo au wazinzi. Ninakushukuru kwa kuwa mimi ni bora kuliko huyu mtoza ushuru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: ‘Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtozaushuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule Farisayo, akiwa amesimama peke yake, akasali hivi: ‘Mungu, ninakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine: Wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule Farisayo, akasimama, akasali hivi na kuomba kwake mwenyewe: ‘Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang’anyi, wadhalimu, na wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: ‘Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: Walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtozaushuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fariseo akasimama, akaomba na kusema hivi moyoni mwake: Mungu, nakushukuru, kwa sababu sifanani na watu wengine walio wanyang'anyi, wapotovu, wagoni, wala sifanani na huyu mtoza kodi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule Mufarisayo akajitenga na mwenzake akiomba hivi: ‘Ee Mungu, ninakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wote wengine wanaokuwa wanyanganyi, watenda maovu, wazinzi. Ninakushukuru vilevile kwa kuwa mimi si kama huyu mulipishaji wa kodi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru.