Luke 18:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia, “Katika mji mmoja palikuwa hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akasema, “Kulikuwa na mwamuzi katika mji fulani. Hakumcha Mungu wala hakujali watu walikuwa wanamfikiriaje.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwepo hakimu ambaye hakumwogopa Mwenyezi Mungu wala kumjali mtu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Palikuwa na hakimu katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Katika mji fulani mlikuwa na mwamuzi asiyemwogopa Mungu, wala hakumcha mtu ye yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akasema: “Katika muji mumoja, kulikuwa mwamuzi mumoja asiyemwogopa Mungu wala kumujali na mutu yeyote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani; hamchi Mungu wala hajali mtu.