Luke 18:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Yesu alizungumza na mitume wake kumi na mbili wakiwa peke yao. Akawaaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu. Kila kitu ambacho Mungu aliwaambia manabii waandike kuhusu Mwana wa Adamu kitatokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawachukua wale Kumi na Wawili, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii yatatimizwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Akawatwaa wale kumi na wawili, akawaambia: Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu. Huko Mwana wa mtu aliyoandikiwa na wafumbuaji yatatimizwa yote:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akawatwaa wanafunzi wake kumi na wawili pembeni, akawaambia: “Tunapanda kwenda Yerusalema, na maneno yote yaliyoandikwa na manabii juu ya Mwana wa Mutu yatatimizwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii.