Luke 18:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wao hawakuelewa jambo hilo hata kidogo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Isa alikuwa anazungumzia nini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mitume walijaribu kulielewa hili, lakini hawakuweza; maana yake ilifichwa wasiielewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wao hawakuelewa jambo hilo hata kidogo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazungumzia nini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Isa alikuwa anazungumzia nini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wao hawakuelewa jambo hilo hata kidogo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hao hawakuyasikia haya hata kidogo, neno hili likawa limefichika, wasilijue maana, wasiyatambue yaliyosemwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini hawakuelewa maneno hayo hata kidogo, na jambo hilo lilikuwa limefichwa kwao, wala hawakufahamu yaliyonenwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wake hawakufahamu maana ya maneno hayo, kwa sababu yalikuwa yamefichwa kwao, nao hawakutambua kama Yesu alisema juu ya nini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao hawakufahamu haya hatta kidogo, neno hili likawa limefichwa kwao, wala hawakuyajua yaliyonenwa.