Luke 19:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, ufalme wa Mungu ungefika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wanasikiliza haya, Isa akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kundi la watu walipokuwa bado wanamsikiliza Yesu akizungumza mambo haya. Akaongeza kwa kuwasimulia simulizi hii. Na sasa alikuwa karibu na mji wa Yerusalemu na watu walidhani kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa unakwenda kutokea haraka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. (Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, Ufalme wa Mungu ungefika.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, ufalme wa Mungu ungefika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa Ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa iyo hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa wanasikiliza haya, Isa akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa Ufalme wa Mwenyezi Mungu ulikuwa unakuja saa iyo hiyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati watu walipokuwa bado wanasikiliza hayo, Yesu akawaambia mfano. Hapo alikuwa anakaribia Yerusalemu, na watu wale walidhani kwamba muda si muda, ufalme wa Mungu ungefika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Watu walipoyasikia hayo, akaongeza kusema na kutoa mfano. Kwa sababu alikuwa karibu ya Yerusalemu, watu wakawaza kwamba: Ufalme wa Mungu sharti utokee sasa hivi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu walipokuwa wakisikiliza maneno hayo, Yesu akaongeza kuwaambia mufano mumoja, kwa sababu alikuwa karibu na muji Yerusalema, na watu wale walizani kwamba siku za Ufalme wa Mungu zitafika saa ile ile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wakisikia haya akaongeza akawaambia mfano, kwa sababu alikuwa akikaribia Yerusalemi, nao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana marra moja.