Luke 19:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo akawaambia, “Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akasema, “Mtu mmoja maarufu alikuwa anajiandaa kwenda katika nchi ya mbali kutawazwa kuwa mfalme. Kisha arudi nyumbani na kuwatawala watu wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo akawaambia, “Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo akawaambia, “Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo akawaambia, “Kulikuwa na mtu mmoja wa ukoo wa kifalme aliyefanya safari kwenda nchi ya mbali ili apokee madaraka ya ufalme, halafu arudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo akasema: Mtu wa kifalme alikwenda kufika katika nchi ya mbali, ajipatie ufalme, kisha arudi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi akasema: “Mutu mumoja mwenye heshima alifunga safari kwenda katika inchi ya mbali kusudi asimikwe kuwa mufalme na kisha arudie.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akasema, Mtu mmoja, mungwana, alisafiri kwenda inchi ya mbali illi kujipatia ufalme na kurejea.