Luke 19:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kabla ya kuondoka, aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kuwaambia: ‘Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake, na akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi hadi nitakaporudi.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo aliwaita watumishi wake kumi kwa pamoja. Akampa kila mtumishi fungu la pesa. Akamwambia kila mtumishi, ‘Zifanyie biashara pesa hizi mpaka nitakaporudi.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kabla ya kuondoka aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kumwambia: Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kabla ya kuondoka, aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kuwaambia: ‘Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi mpaka nitakaporudi.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake, na akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi mpaka nitakaporudi.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hadi nitakaporudi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kabla ya kuondoka, aliwaita watumishi wake kumi, akawapa kiasi cha fedha kila mmoja na kuwaambia: ‘Fanyeni nazo biashara mpaka nitakaporudi.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaita watumwa wake kumi, akawapa mia kumi za shilingi, akawaambia: Zichuuzieni, mpaka nitakaporudi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbele ya kuondoka kwake akawaita watu kumi kati ya watumishi wake, akamupatia kila mumoja furushi moja ya zahabu na kuwaambia: ‘Mufanye nazo uchuuzi mpaka nitakaporudia.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaita watu kumi katika watumishi wake, akawapa mane za fedha kumi, akawaambia, Fanyeni biashara hatta nitakaporudi.