Luke 19:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na kuchuma ambacho hukupanda.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mgumu. Unachukua ambapo hukuweka, na kuvuna ambapo hukupanda.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Niliogopa kwa sababu wewe ni mgumu. Unachukua hata pesa ambazo hukuzizalisha na kukusanya chakula ambacho hukupanda.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na huchuma ambacho hukupanda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na kuchuma ambacho hukupanda.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mgumu. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mgumu. Unachukua ambapo hukuweka kitu, na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; wachukua usichoweka, wavuna usichopanda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Wewe ni mtu ambaye huchukua yasiyo yako, na kuchuma ambacho hukupanda.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani nilikuogopa, kwa kuwa wewe u mkorofi, hutwaa usiyoyaweka, huvuna usioyoyapanda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa maana nilikuogopa kwa maana wewe ni mutu mugumu. Unatafutia nafasi usipowekea na kuvuna nafasi usipopanda.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
maana nalikuogopa, kwa sababu wewe mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.