Luke 19:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na sasa, kuhusu hao maadui zangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao. Waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa, adui zangu wako wapi? Wako wapi watu ambao hawakutaka niwe mfalme? Waleteni adui zangu hapa na waueni huku nikiangalia wanavyokufa.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na sasa, kuhusu hao maadui wangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na sasa, kuhusu hao maadui zangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao, waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao. Waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa muwachinje mbele yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na sasa, kuhusu hao maadui zangu ambao hawapendi niwe mfalme wao, waleteni hapa, mkawaue papa hapa mbele yangu.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wale wachukivu wangu wasionitaka, niwatawale, mwalete hapa, mwachinje mbele yangu!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sasa kwa ngambo ya wale waadui zangu walionikataa mimi kuwa mufalme wao, muwalete hapa na kuwaua mbele yangu.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walakini wale adui zangu wasiotaka niwatawale, waleteni huku mkawachinje mhele zangu.