Luke 19:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwanapunda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtampata mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
akawaambia, “Nendeni kwenye mji mnaoweza kuuona pale. Mtakapoingia mjini, mtamwona mwanapunda amefungwa ambaye bado mtu yeyote hajampanda. Mfungueni na mleteni hapa kwangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana punda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungeni, mkamlete hapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwanapunda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nendeni katika kijiji kile kilicho mbele yenu, mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda ambaye hajapandwa na mtu bado, akiwa amefungwa hapo. Mfungueni, mumlete hapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akisema, Nendeni mpaka katika kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwanapunda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu yeyote bado, mfungueni mkamlete hapa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akawaambia: “Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwanapunda amefungwa ambaye hajatumiwa na mtu. Mfungueni, mkamlete hapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akisem: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mtakapoingia mle mtaona, pamefungwa mwana punda, ambaye mtu hajampanda bado; mfungueni, mmlete!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akisema, Nendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwana-punda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu ye yote bado, mfungueni mkamlete hapa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwende katika kijiji kinachokuwa mbele yenu. Mutakapofika kule, mutaona mwana-punda amefungwa, na hakuna mutu aliyekwisha kupanda juu yake. Mumufungue na kumuleta hapa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakabili ninyi, na mkiingia ndani, mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni.