Luke 2:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Rumi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ulikuwa wakati ambapo amri ilitolewa na Kaisari Augusto kwamba watu wote wanaoishi katika utawala wote wa Rumi wahesabiwe na kuorodheshwa katika kumbukumbu za serikali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote chini ya utawala wake wajiandikishe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ikawa siku zile, amri ikitoka kwa Kaisari Augusto, walimwengu wote waandikiwe kodi;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile, Augusto, mufalme wa Roma akatoa amri kwamba wafanye hesabu ya watu wa utawala wake wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HATTA siku zile kulitoka amri kwa Kaisari Augusto ya kama iandikwe orodha ya majina ya walimwengu wote: