Luke 2:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya yaliyotukia, ambayo Mwenyezi Mungu ametuambia habari zake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika walipoondoka kurudi mbinguni, wale wachungaji wakaambiana wakisema, “Twendeni Bethlehemu, tukalione jambo hili lililotokea, ambalo Bwana ametujulisha.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao wakisema, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Bwana ametuambia habari zake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Mwenyezi Mungu ametuambia habari zake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ikawa, malaika walipoondoka kwao kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezana wao kwa wao: Haya! Twende, tufike hata Beti-Lehemu, tulitazame jambo hilo lililokuwapo, Bwana alilotutambulisha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wamalaika walipoondoka na kurudia mbinguni, wachungaji wakasemezana: “Basi tuende Betelehemu, kusudi tupate kuona jambo lile lililotokea, ambalo Bwana alitujulisha.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa malaika walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakaambiana, Haya na twende zetu mpaka Bethlehemu, tukaone neno hili lililofanyika, Bwana alilotujulisha.