Luke 2:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wachungaji waliirudia mifugo yao, wakawa wanamsifu na kumshukuru Mungu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona. Ilikuwa kama walivyoambiwa na malaika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wachungaji wakarudi wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa yote, waliyoyasikia, kwani waliona, ni vivyo, kama walivyoambiwa.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wachungaji wakarudia wakitukuza Mungu na kumusifu kwa ajili ya mambo yote waliyoyasikia na kuyaona, kwa maana yote yalifanyika sawa vile malaika alivyokuwa amewaambia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wachungaji wakarudi, wakimtukuza Mungu na kumhimidi kwa mambo yote waliyosikia, na waliyoona, kwa namna waliyoambiwa.