Luke 2:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na sheria, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele za Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulipotimia wakati wa utakaso wake Mariamu kwa mujibu wa Torati ya Musa, basi Yusufu na Mariamu walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Muda wa kutakaswa ulimalizika, kama ilivyotakiwa na Sheria ya Musa baada ya mtoto kuzaliwa. Baada ya hapo walimpeleka Yesu Yerusalemu na kumweka mbele za Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na Sheria ya Mose, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na sheria, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele za Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulipotimia wakati wa utakaso wake Maria, kwa mujibu wa Sheria ya Mose, Yosefu na Maria walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Bwana,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulipotimia wakati wa utakaso wake Mariamu kwa mujibu wa Torati ya Musa, basi Yusufu na Mariamu walimpeleka mtoto Yerusalemu, ili kumweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo Torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na sheria, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele za Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Siku zao zilipotimia za weuo, aliouagiza Mose, wakampeleka Yerusalemu, wamtokeze kwake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku zilipotimia za Maria na Yosefu kutakaswa kama vile Sheria ya Musa inavyoagiza, wakamupeleka mutoto Yerusalema, kusudi wapate kumutolea kwa Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nazo siku za kutakasika kwao zilipotimia, kwa sharia ya Musa, wakamleta Yerusalemi, wampe Bwana;