Luke 2:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia walikwenda ili watoe sadaka: Hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika sheria ya Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Torati ya Mwenyezi Mungu: “Hua wawili au makinda wawili wa njiwa”.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia Mariamu na Yusufu walikwenda Yerusalemu kutoa dhabihu kama Sheria ya Bwana inavyosema kuwa, “Ni lazima utoe dhabihu ya jozi moja ya hua au makinda mawili wa njiwa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda wawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia walikwenda ili watoe sadaka: hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika sheria ya Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa, katika Sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda mawili ya njiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na pia kutoa dhabihu kulingana na yale yaliyonenwa katika Torati ya Bwana Mwenyezi: “Hua wawili au makinda mawili ya njiwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia walikwenda ili watoe sadaka: Hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika sheria ya Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakatoa vipaji vya kumkomboa, kama ilivyoagizwa katika Maonyo ya Bwana, hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakatoa vilevile sadaka sawa vile inavyoagizwa katika Sheria ile: “Hua wawili au vitoto viwili vya njiwa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakatoe sadaka kama ilivyonenwa katika sharia ya Bwana, Hua wawili, au makinda ya njiwa mawili.