Luke 2:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na sheria,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Simeoni, akiwa ameongozwa na Roho wa Mungu, alienda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Isa ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Torati,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho Mtakatifu alimwongoza mpaka Hekaluni. Hivyo, alikuwemo Hekaluni wakati Mariamu na Yusufu walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyotakiwa katika Sheria ya Kiyahudi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia Hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta Hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na Sheria,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na sheria,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Simeoni akiwa ameongozwa na Roho Mtakatifu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Sheria,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Simeoni, akiwa ameongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Isa ili kumfanyia kama ilivyokuwa desturi ya Torati,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na sheria,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, akaja Patakatifu kwa kuongozwa na Roho. Wazazi walipoingia na mtoto Yesu, wamfanyie, kama walivyozoezwa na Maonyo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ilimutokea Simeoni kuingia ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho. Wazazi walipomuleta mutoto wao Yesu kusudi wamutendee sawa ilivyoagizwa na Sheria,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi akaja hekaluni kwa roho: na wazee wake walipomleta mtoto Yesu, wamfanyie kwa desturi ya sharia,