Luke 2:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu; “Wayahudi wengi wataanguka na wengi watainuka kwa sababu ya mtoto huyu. Atakuwa ishara kutoka kwa Mungu, lakini baadhi ya watu watamkataa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Simeoni akawabariki, akamwambia Maria, mama yake: Tazama, huyu ndiye aliyewekewa, wengi walio Waisiraeli waangushwe naye, nao wengine wengi wainuliwe naye; tena amewekewa kuwa kielekezo kinachobishiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simeoni akawabariki na kumwambia Maria, mama yake: “Mutoto huyu amezaliwa kwa sababu ya kuwaangusha na kuwasimamisha watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa kitambulisho kutoka kwa Mungu watu watakachokipinga,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;