Luke 2:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwapo nabii aliyeitwa Ana binti Fanueli, kutoka katika kabila la Asheri. Alikuwa mwanamke mzee sana. Aliishi na mume wake kwa miaka saba,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke mzee sana, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana, naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Palikuwa na nabii mwanamke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kukawa na mfumbuaji wa kike, jina lake Ana, binti Fanueli, wa shina la Aseri. Huyo miaka yake ilikuwa mingi sana; alikuwa amekaa pamoja na mumewe miaka saba baada ya kuwa manamwali.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa vilevile nabii mumoja mwanamuke, aliyeitwa Ana, aliyekuwa binti ya Fanueli, wa kabila la Aseri. Yeye alikuwa muzee sana. Aliishi miaka saba na mume wake tangu alipoolewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kulikuwa na Auna, nabii mke, binti Fanueli, wa kabila ya Asher; nae kongwe wa siku nyingi, amekuwa na mume miaka saba baada ya ujana wake;