Luke 2:44 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wao wakidhani kuwa yuko miongoni mwa wasafiri, walienda mwendo wa kutwa nzima. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na rafiki zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walianza kumtafuta kwa jamaa na rafiki zao baada ya kusafiri kutwa nzima, wakidhani kuwa alikuwa pamoja nao katika msafara.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wao wakidhani kuwa yuko miongoni mwa wasafiri, walienda mwendo wa kutwa nzima. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa zao na marafiki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wao wakidhani kuwa yuko miongoni mwa wasafiri, walienda mwendo wa kutwa nzima. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa zao na marafiki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakadhani, yumo katika wenzake wa njiani. Wakaenda mwendo wa siku moja, kisha wakamtafuta kwa ndugu zao na kwa wenzi wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walizania kama alikuwa pamoja na wenzake aliosafiri nao. Kisha kutembea mwendo wa siku nzima, wakaanza kumutafuta katikati ya wandugu zao na ya watu waliojuana nao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakadhani yumo katika msafara yao, wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao,