Luke 2:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori la kulia ng’ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akamzaa mwanawe wa kwanza. Akamvingirishia nguo vizuri, kisha akamlaza katika hori la kulishia mifugo. Walimweka humo kwa sababu chumba cha wageni kilikuwa kimejaa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamzaa mwana wake wa kwanza, ni wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza waliamo ng'ombe, kwani hawakupata pengine nyumbani mwa wageni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akazaa mwana, ndiye muzaliwa wake wa kwanza. Akamufunika nguo za kitoto na kumulalisha katika sanduku ya kukulishia nyama, kwa sababu walikosa nafasi ya kukaa katika nyumba ya kupangisha wageni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamzaa mtoto wake wa kifungua mimba, akamfunga nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakuona nafasi katika nyumba ya wageni.