Luke 2:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula tazama, malaika wa Mwenyezi Mungu akawatokea, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukawang’aria kotekote, wakaingiwa na hofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukaangaza kuwazunguka, wakaogopa sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawang'aria kotekote, wakaingiwa na hofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula tazama, malaika wa Mwenyezi Mungu akawatokea, nao utukufu wa Bwana Mwenyezi ukawang’aria kotekote, wakaingiwa na hofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndiko, malaika wa Bwana alikowatokea, nao utukufu wa Bwana ukawamulikia po pote, wakashikwa na woga mwingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa rafla malaika wa Bwana akawatokea, na mwangaza wa utukufu wa Bwana ukawazunguka. Nao wakaogopa sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa Bwana akawatokea, utukufu wa Bwana ukawangʼaria: wakaingiwa na khohi nyingi.