Luke 20:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na waalimu wa sheria pamoja na wazee walifika,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja, Isa alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri Habari Njema, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, pamoja na wazee wa watu wakamjia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku moja Yesu alikuwa anawafundisha watu katika eneo la Hekalu. Alikuwa anawahubiri Habari njema. Viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na viongozi wazee wa Kiyahudi walikwenda kuzungumza na Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na walimu wa Sheria pamoja na wazee walifika,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na waalimu wa sheria pamoja na wazee walifika,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wakamjia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja, Isa alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, pamoja na wazee wa watu wakamjia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri Habari Njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafla;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuwahubiria juu ya Habari Njema, makuhani wakuu na waalimu wa sheria pamoja na wazee walifika,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa siku moja, alipofundisha watu hapo Patakatifu na kuipiga hiyo mbiu njema, wakamwinukia watambikaji wakuu na waandishi na wazee,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni, na kuihubiri habari njema, wakuu wa makuhani na waandishi pamoja na wazee walimtokea ghafula;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Yesu alikuwa katika hekalu akiwafundisha watu na kuhubiri Habari Njema. Wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria pamoja na wasimamizi wa watu wakamufikia na kumwuliza:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
IKAWA siku moja, alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuikhubiri Injili, makuhani wakuu na waandishi, na pamoja nao wazee, wakamtokea ghafula,