Luke 20:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo, wakamrudisha mikono mitupu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wa kuvuna zabibu ulipofika, alimtuma mmoja wa watumishi wake kwa wakulima wale ili wampe sehemu yake ya zabibu. Lakini wakulima wale walimpiga yule mtumishi na wakamfukuza bila kumpa kitu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo wakamrudisha mikono mitupu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo, wakamrudisha mikono mitupu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati wa mavuno akamtuma mtumishi wake kwa hao wakulima aliowakodishia ili wampatie sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima waliokodisha wakampiga na kumfukuza mikono mitupu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa mavuno, mtu huyo alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima, akachukue sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga mtumishi huyo, wakamrudisha mikono mitupu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zilipotimia, akatuma mtumwa kwa wale wakulima, wampe matunda ya mizabibu. Lakini wakulima wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku za mavuno zilipotimia, akamutuma mutumishi wake mumoja kwa wale walimaji kusudi wamupatie sehemu yake ya mavuno. Lakini wale walimaji wakamupiga na kumurudisha mikono mitupu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wakati wa mavuno akatuma mtumishi kwa wale wakulima illi wampe baadhi ya matunda ya mizabibu, wakulima wakampiga, wakamtoa hana kitu.