Luke 20:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; na ye yote ambaye litamwangukia litamsaga kabisa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika na ikiwa jiwe hilo litaangukia, litakusaga!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo, atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamsaga kabisa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande na ye yote litakayemwangukia litamsagasaga awe unga.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika; na yeyote ambaye litamwangukia litamsaga kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote akianguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kila atakayeanguka juu ya jiwe lile atapondeka; naye litakayemwangukia, litambana tikitiki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; na ye yote ambaye litamwangukia litamsaga kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mutu atakayeanguka juu ya jiwe lile, atavunjika na yule litakayemwangukia, litamuponda.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Killa mtu aangukae juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika, nae ambae litamwangukia litamsagasaga.