Luke 20:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waalimu wa sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walimu wa Torati na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta kumkamata saa iyo hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walimu wa sheria na wakuu wa makuhani waliposikia kisa hiki, walijua unawahusu wao. Hivyo walitaka kumkamata Yesu wakati huo huo, lakini waliogopa watu wangewadhuru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walimu wa Sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waalimu wa sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walimu wa sheria na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja kwa sababu walifahamu kwamba ametoa mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walimu wa Torati na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao waandishi na wakuu wa makuhani walitaka kumkamata saa hiyo hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waalimu wa sheria na makuhani wakuu walifahamu kwamba mfano huo ulikuwa unawahusu, na hivyo walitaka kumkamata palepale, ila tu waliogopa watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Saa ileile waandishi na watambikaji wakuu wakatafuta kumkamata, lakini waliliogopa lile kundi la watu; kwani walitambua, ya kuwa amewasemea wao wenyewe mfano lhuo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta kumkamata saa iyo hiyo, wakawaogopa watu, maana walitambua ya kwamba mfano huu amewanenea wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saa ile ile wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria wakatafuta kumukamata, kwa sababu walitambua kwamba alisema mufano huo juu yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata saa hiyo hiyo, wakawaogopa watu: maana walitambua ya kuwa ule mfano amewanena wao.