Luke 20:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo wale watu wakamwambia Yesu, “Mwalimu, tunafahamu kwamba yale unayosema na kufundisha ni kweli. Haijalishi ni nani anasikiliza, unafundisha sawa kwa watu wote. Daima unafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wale wapelelezi wakamwuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu kwa kufuata ukweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao wapelelezi wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli; tunajua kwamba wewe huna ubaguzi; wewe wafundisha ukweli juu ya njia ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakamwuliza wakisema: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa unasema ya kweli na kuyafundisha, hutazami nyuso za watu, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, twajua ya kwamba wasema na kufundisha yaliyo ya haki, wala hujali cheo cha mtu, bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wapelelezi wakamwuliza: “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha maneno ya kweli. Vilevile wewe hauangalii cheo cha mutu, lakini unafundisha juu ya namna ya kuishi ambayo Mungu anaamuru kufuata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamwuliza, wakinena, Mwalimu, twajua ya kuwa wanena yaliyo kweli na kuyafundisha, wala hujali cheo cha mtu, bali katika kweli waifundisha njia ya Mungu: