Luke 20:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wale wakashangaa jibu lake la hekima. Hawakusema kitu. Hawakuweza kumtega Yesu pale mbele za watu. Hakusema chochote kibaya ambacho wangekitumia ili kumnasa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza kimya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza kimya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hawakufaulu kumnasa kwa neno lolote pale mbele ya watu na hivyo wakakaa kimya wakilistaajabia jibu lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo hawakuweza kumnasa kwa maneno yake mbele za watu, wakamstaajabu, alivyojibu, wakanyamaza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hawakuweza kumshitaki kwa maneno yake mbele ya watu; wakastaajabia majibu yake, wakanyamaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi watu wale hawakuweza kumunasa katika neno lolote mbele ya watu, lakini wakashangaa na jibu lake, nao wakanyamaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala hawakuweza kumshika kwa neno lake mbele ya watu: wakastaajabia jawabu lake, wakanyamaza.