Luke 20:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Mwalimu, Musa aliandika kwamba mtu aliyeoa akifa na hakuwa na watoto, kaka au mdogo wake amwoe mjane wake, ili wawe na watoto kwa ajili ya yule aliyekufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, amzalie watoto ndugu yake marehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kuacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu ya mtu fulani akifa na kumwacha mjane wake bila watoto, ni lazima ndugu yake amchukue huyo mama mjane, ili ampatie ndugu yake watoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfunzi, Mose alitundikia: Mtu akifiwa na mkubwa wake aliyekuwa na mkewe pasipo kuwa na mwana, nduguye amchukue huyo mke, amzalie mkubwa wake mwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwalimu, Musa alituamuru: Mutu akiwa na ndugu yake, naye akikufa na kuacha muke wake bila mutoto, yule ndugu yake anapaswa kumwoa yule mujane na kumuzalia ndugu yake marehemu watoto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwalimu, Musa alituandikia ya kama ndugu ya mtu akifa, nae ana mke, na mtu huyo akifa hana mtoto, ni lazima ndugu yake amtwae yule mke, akampatie ndugu yake mzao.