Luke 20:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Mwenyezi Mungu, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Musa alionesha dhahiri kwamba watu hufufuliwa kutoka kwa wafu. Alipoandika kuhusu kichaka kilichokuwa kinaungua, alisema kwamba Bwana ni ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana ‘Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana Mwenyezi Mungu, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionesha katika sura ya Kichaka, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, kwamba kuna kufufuka kutoka kwa wafu, hata Mose alithibitisha jambo hilo katika Maandiko Matakatifu. Katika sehemu ya Maandiko Matakatifu juu ya kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto, anamtaja Bwana kama Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwa ajili ya wafu, kwamba wafufuliwa, hata Mose alivifumbua kidogo hapo kichakani alipomwita Bwana: Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musa alionyesha waziwazi kwamba wafu watafufuka. Katika maandiko yake yanayosema juu ya kichaka kilichowaka moto, yeye anamutaja Bwana kuwa ni ‘Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walakini ya kuwa wafu wafufuka, Musa nae alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo amtajapo Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaak, na Mungu wa Yakobo.