Luke 20:46 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jilindeni na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Iweni waangalifu dhidi ya walimu wa sheria. Wanapenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yanayoonekana ya heshima. Na wanapenda pale watu wanapowasalimu kwa heshima maeneo ya masoko. Wanapenda kukaa sehemu za heshima katika masinagogi na sehemu za watu maarufu katika sherehe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Jihadharini na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa majoho marefu na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hukaa kwenye viti maalum katika masinagogi na kukaa kwenye sehemu za wageni wa heshima katika karamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jilindeni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni! Namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele, hata wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jilindeni na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mujiepushe na walimu wa Sheria wanaopenda kujitembeza, wakivaa kanzu ndefu na kusalimiwa kwa heshima kwenye nafasi za makutano. Wanapenda vilevile kuikaa katika viti vya mbele ndani ya nyumba za kuabudia, na kwenye nafasi za heshima katika karamu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jihadharini na waandishi wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika sunagogi, na mahali palipo mbele katika karamu.