Luke 20:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawaambia watu kisa hiki; “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Kisha akalikodisha kwa wakulima, kisha akasafiri kwa muda mrefu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba lake la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akakondisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima; kisha akasafiri hadi nchi ya mbali, akakaa huko kwa muda mrefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaanza kuwatolea watu mfano huu: Mtu alipanda mizabibu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine kukaa siku nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaendelea kuwaambia watu mufano huu: “Mutu mumoja alipanda shamba la mizabibu. Kisha kupatana kugawanyana mavuno na walimaji wamoja watakaobaki wakitunza shamba lake, akaenda safari katika inchi ingine na kukaa kule kwa muda murefu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaanza kuwaambia watu mfano huu: Mtu alipanda mizabibu, akapangisha wakulima, akaenda inchi nyingine kwa muda wa siku nyingi.