Luke 21:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, na njaa kali, na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali. Pia kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kutakuwa matetemeko makubwa, kutakuwa njaa na magonjwa ya kutisha sehemu nyingi. Mambo ya kutisha yatatokea, na mambo ya kushangaza yatatokea kutoka mbinguni ili kuwaonya watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, kutakuwa na njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutakuwa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali, njaa kali na magonjwa ya kuambukiza. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, na njaa kali, na magonjwa ya kuambukiza katika sehemu mbalimbali. Pia kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi; na njaa na tauni mahali pengi; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mahali kutakuwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi, njaa na tauni. Kutakuwa na vituko vya kutisha na ishara kubwa angani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali penginepengine patakuwa na matetemeko makuu, pengine na kipindupindu, pengine na njaa. Hata vielekezo vikubwa vitatokea mbinguni vya kuogofya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutakuwa tetemeko kubwa la inchi. Vilevile kutakuwa njaa na magonjwa makali kwenye nafasi mbalimbali. Zaidi ya ile kutakuwa mambo ya kuogopesha na vitambulisho vya ajabu toka mbinguni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kutakuwa na matetemeko makubwa ya inchi mahali mahali, na njaa, na tauni. Kutakuwa na mambo ya kutisha, na ishara kuu kutoka mbinguni.