Luke 21:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo, wale walio Yudea wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo, nao wale walio mashambani wasiingie mjini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu walioko katika Uyahudi wakati huo wakimbilie milimani. Mtu yeyote atakaye kuwa Yerusalemu wakati huo aondoke haraka. Ikiwa utakuwa karibu na mji, usiingie mjini!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo, wale walio Uyahudi wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo na wale walioko mashambani wasiingie mjini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo, wale walio Uyahudi wakimbilie milimani, walio mjini Yerusalemu watoke humo, nao wale walioko mashambani wasiingie mjini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo walio katika Yudea na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, walioko Yudea wakimbilie milimani; wale walio mjini watoke; na wale walio mashambani wasirudi mjini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani! Nao watakaokuwamo mle mjini watoke! Nao watakaokuwako shambani wasiuingie tena!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wale watakaokuwa Yudea, wakimbilie kwa milima, na wale watakaokuwa Yerusalema watoke ndani yake, nao wale watakaokutiwa katika mashamba wasiingie ndani ya muji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani, na walio katikati yake watoke waende zao, na walio shambani wasiuingie.