Luke 21:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati huu utakuwa mgumu kwa wanawake wenye mimba au wanaonyonyesha watoto wadogo, kwa sababu mambo mabaya yatakuja katika nchi hii. Mungu atawaadhibu watu wake kwa sababu wamemkasirisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wao wenye mimba na watakaokuwa wananyonyesha katika siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! Kutakuwa na dhiki kuu katika nchi na ghadhabu juu ya hawa watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wao waja wazito na wanyonyeshao siku hizo! Kwa maana kutakuwa na dhiki kubwa katika nchi, na hasira ya Mungu itawajia watu hawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watakaoona vibaya zaidi ndio wenye mimba na wenye kunyonyesha siku zile. Kwani itakuwa kondo kubwa katika nchi, makali yatakapowatokea watu wa kabila hili:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanawake wenye mimba na wenye kunyonyesha watapata hasara katika siku zile! Kwa maana kutakuwa taabu kubwa katika inchi, na Mungu ataonyesha kasirani yake juu ya watu wa taifa hili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku zile! kwa maana itakuwa shidda kuu juu ya inchi, na ghadhabu juu ya watu hawa.