Luke 21:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wataanguka kwa makali ya upanga, na wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote. Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya watu watauawa, wengine watafanywa watumwa na kuchukuliwa katika nchi mbalimbali. Mji mtakatifu wa Yerusalemu utatekwa na kuwekwa chini ya utawala wa wageni mpaka wakati ulioruhusiwa wao kufanya hivi utakapokwisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wataanguka kwa makali ya upanga, wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote, nao Yerusalemu utakanyagwa na watu Mataifa hadi muda wa hao watu Mataifa utimie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wataanguka kwa makali ya upanga, na wengine watachukuliwa kuwa mateka katika mataifa yote. Nao mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa Mataifa hadi muda wa hao watu wa Mataifa utimie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hadi majira ya Mataifa yatakapotimia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wengine watauawa kwa upanga, wengine watachukuliwa mateka katika nchi zote; na mji wa Yerusalemu utakanyagwa na watu wa mataifa mengine, hadi nyakati zao zitakapotimia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wengine wataanguka kwa ukali wa panga, wengine watatekwa na kutawanyishwa kwenye mataifa yote. Namo Yerusalemu mtakanyagwa na wamizimu, mpaka siku za wamizimu zitakapotimizwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wamoja watauawa kwa vita na watapelekwa kuwa wafungwa katika inchi za mataifa yote. Vilevile mataifa mengine yatautawala Yerusalema mpaka nyakati zao za kuutawala zitakapokwisha.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wataanguka kwa ukali wa upanga, watachukuliwa mateka mpaka mataifa yote: nao Yerusalemi utakanyagwa na mataifa, hatta majira ya mataifa yatakapotimia.