Luke 21:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba majira ya mavuno yamekaribia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Unapochipua majani mnatambua kwamba majira ya joto yamekaribia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba majira ya mavuno yamekaribia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati imalizapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba majira ya mavuno yamekaribia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mnapoiona, ikichipua, mnatambua wenyewe, ya kuwa siku za vuli zimekwisha kuwa karibu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munapoona kwamba majani yao yanaanza kuchipuka, munatambua wenyewe kwamba wakati wa jua kali unakaribia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
iishapo kuchupua, mwaona na kutambua nafsini mwenu ya kwamba mavuno yameisha kuwa karibu.