Luke 21:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali yao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale wanavyo vingi, na wametoa vile ambavyo hawavihitaji. Lakini mwanamke huyu ni maskini sana, lakini ametoa vyote alivyokuwa akitegemea ili aishi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kwa Mungu kutokana na wingi wa mali zao, lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo kwa ajili ya maisha yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
maana, hao wote walitoa sadaka katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana, wengine wote wametoa sadaka zao kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hao wote walitoa mali katika mali zao nyingi, wakazitia penye sadaka, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vilivyomlisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana hawa wengine wote walitoa sehemu ya mali wasiyokuwa nayo lazima. Lakini yeye ametoa kwa umasikini wake mali yote aliyokuwa nayo kwa kuishi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa maana hawa wote wametia katika sadaka za Mungu baadhi ya mali iliyowazidi, bali huyu katika mahitaji yake ametia vitu vyote alivyokuwa navyo.