Luke 21:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Haya yote mnayoyaona — zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yesu akasema, “Wakati utafika ambao yote mnayoyaona hapa yatateketezwa. Kila jiwe katika majengo haya litatupwa chini. Hakuna jiwe litakaloachwa juu ya jingine.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Haya yote mnayoyaona—zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Haya yote mnayoyaona — zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalosalia juu ya jiwe jingine, kila moja litabomolewa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kuhusu haya mnayoyaona hapa, wakati utafika ambapo hakuna jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali kila moja litabomolewa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Haya yote mnayoyaona – zitakuja siku ambapo hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitaharibiwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Mwayatazama haya? Siku zitakuja, ambapo halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kutakuwa siku vitu hivi munavyoona vitabomolewa, wala hakutabaki hata jiwe moja juu ya lingine.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Haya mnayoyatazama, siku zitakuja, halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.