Luke 21:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamuuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatukia lini? Ni dalili gani itaonesha kwamba yanakaribia kutendeka?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya watu wakamwuliza Yesu, “Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Dalili ipi itatuonyesha kwamba ni wakati wa mambo haya kutokea?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonyesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatukia lini? Ni dalili gani zitaonyesha kwamba yanakaribia kutendeka?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamuuliza, “Mwalimu, mambo haya yatatukia lini? Ni dalili gani itaonyesha kwamba yanakaribia kutendeka?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo yako karibu kutukia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamwuliza, “Mwalimu, mambo hayo yatatokea lini? Na ni ishara gani zitakazoonesha kwamba karibu mambo hayo yatokee?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwuliza wakisema: Mfunzi, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo ni nini, hayo yatakapotimia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakamwuliza: “Mwalimu, mambo hayo unayotoka kusema yatakuwa wakati gani? Na ni kitambulisho gani kitakachoonyesha kwamba yanataka kutimia?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakuimwuliza, wakisema, Mwalimu, haya yatakuwa lini, bassi? Na nini dalili ya kuwa haya yote ni karibu ya kutimia?