Luke 21:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Iweni waangalifu, msije mkarubuniwa. Watu wengi watakuja wakitumia jina langu, watasema, ‘Mimi ndiye Masihi,’ na ‘Wakati sahihi umefika!’ Lakini msiwafuate.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu wakisema: Mimi ndiye, na, Wakati ule umekaribia. Lakini ninyi msiwafuate!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai kwamba, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akasema: Angalieni, msipotezwe! Kwani wengi watakuja kwa Jina langu na kusema: Mimi ndiye, nazo siku zimekwisha kufika. Msiwafuate hao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawajibu: “Muangalie vizuri, musidanganywe. Watu wengi watakuja wakijiita kwa jina langu, wakisema kwamba wao ndio Kristo, nao wakati umetimia. Ingawa vile, musiwafuate.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.