Luke 22:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akafanya vivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika namna ile ile, baada ya kula chakula, Yesu akachukua kikombe chenye divai na akasema, “Divai hii inawakilisha Agano Jipya kutoka kwa Mungu kwa watu wake. Litaanza pale damu yangu itakapomwagika kwa ajili yenu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada ya chakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akafanya vivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vivyo hivyo baada ya kula, akachukua kile kikombe akasema, “Kikombe hiki ni Agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akafanya vivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo akakitwaa nacho kinyweo, walipokwisha kula, akisema: Kinyweo hiki ndicho Agano Jipya katika damu yangu inayomwagwa kwa ajili yenu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile kisha kula akatwaa kikombe na kuwapa akisema: “Kikombe hiki ni agano jipya la Mungu, linalohakikishwa kwa njia ya damu yangu.]
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nacho kikombe vivyo hivyo baada ya kula, akinena, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.