Luke 22:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana, ni nani aliye mkuu: Yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule anayeketi mezani au ni yule anayehudumu? Si ni yule aliyeketi mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule anayehudumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nani ni mkuu zaidi: Yule anayetumika au yule aliyekaa mezani na kuhudumiwa? Kila mtu hudhani ni yule aliyekaa mezani akihudumiwa, sawa? Lakini nimekuwa pamoja nanyi kama ninayetumika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule aketiye mezani au ni yule ahudumiaye? Si ni yule aliyekaa mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule ahudumiaye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwani ni nani aliye mkuu? Ni yule aketiye mezani au ni yule ahudumuye? Si ni yule aliyekaa mezani? Lakini mimi niko miongoni mwenu kama yule ahudumuye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana, ni nani aliye mkuu: Yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani aliye mkubwa ni yupi? Anayekaa chakulani au anayetumika? Si yule anayekaa chakulani? Lakini mimi kati yenu niko kama mwenye kutumika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana, ni nani anayekuwa mukubwa; yule anayeikaa kwa kula chakula au yule anayemushugulikia? Hakika ni yule anayeikaa kwa kula chakula. Ingawa vile mimi niko hapa katikati yenu kama mwenye kushugulika!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana nani mkubwa, aketiye chakulani, ama akhudumuye?