Luke 22:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe baada ya kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
nimekuombea ili usipoteze imani yako! Wasaidie ndugu zako kuwa imara utakaponirudia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini nimekuombea wewe Simoni ili imani yako isishindwe, nawe ukiisha kunirudia, uwaimarishe ndugu zako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mimi nimekuombea, kunitegemea kwako kusikome. Nawe hapo, utakapogukia, uwatie ndugu zako nguvu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mimi nimekuombea, kusudi usipungukiwe na imani. Nawe utakaponirudilia tena, uwatie wandugu zako moyo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.