Luke 22:42 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Baba, ukiwa radhi, tafadhali usinifanye ninywe katika kikombe hiki. Lakini fanya unalotaka wewe, siyo ninalotaka mimi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki, lakini si kama mimi nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; lakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baba, ukitaka kipitishe kinyweo hiki, nisikinywe! Lakini yasifanyike, niyatakayo mimi, ila yafanyike uyatakayo wewe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Baba, kama ukitaka, ninakuomba uniondolee mbali kikombe cha mateso. Lakini isikuwe mapenzi yangu ndiyo yafanyike, lakini yako.” [
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baba, ukipenda, uniondolee kikombe hiki: lakini si kama nitakavyo mimi, illa utakavyo wewe vifanyike.