Luke 22:44 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliomba kwa nguvu zaidi na kustahimili zaidi kama mpiganaji wa mieleka akiwa katika mapambano makali. Jasho kama matone ya damu likadondoka kutoka kwenye uso wake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka, kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka chini.]
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawa akigombana na kifo, kwa hiyo akajihimiza kuomba, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yaliyodondoka chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alikuwa katika uchungu mukubwa, akazidi kuomba kwa bidii. Jasho iliyomutoka ikakuwa kama matone ya damu yaliyokuwa yakitiririka mpaka chini.]
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae kwa kuwa alikuwa na huzuni sana, akazidi kuomba kwa bidii. Hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka hatta inchi.