Luke 22:47 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu wakaja. Waliongozwa na Yuda, aliyekuwa mmoja wa wale kumi na wawili. Akamkaribia Isa ili ambusu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipokuwa anaongea, kundi likaja. Lilikuwa linaongozwa na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili. Akamwendea Yesu ili ambusu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Yesu alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja, ukiongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Yesu ili ambusu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokuwa bado anazungumza, umati mkubwa wa watu ukaja. Uliongozwa na Yuda, ambaye alikuwa mmoja wa wale wanafunzi Kumi na Wawili. Akamkaribia Isa ili ambusu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Angali akisema, mara wakaja kundi la watu, mmoja wao wale kumi na wawili, jina lake Yuda, akiwatangulia, akamkaribia Yesu kumnonea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa hajamaliza kusema, kundi la watu wakafika, wakiongozwa na Yuda, mumoja wa wanafunzi kumi na wawili. Akamujongelea Yesu kusudi amubusu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae alipokuwa akisema, tazama, makutano, nae aitwae Yuda, mmoja wa wathenashara, akitangulia mbele yao, akamkaribia Yesu kumbusu.