Luke 22:50 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mmoja wao akautumia upanga wake. Akakata sikio la kulia la mtumishi wa kuhani mkuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wao akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kulia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenzao mmoja akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio la kuume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mumoja wao akamupiga mutumishi wa Kuhani Mukubwa upanga na kumukata sikio la kuume.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio la kuume.