Luke 22:52 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyanganyi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Isa akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akaliambia lile kundi lililokuja kumkamata. Walikuwa viongozi wa makuhani, viongozi wa wazee wa Kiyahudi na askari walinzi wa Hekalu. Akawaambia, “Kwa nini mmekuja hapa mkiwa na mapanga na marungu? Mnadhani mimi ni mhalifu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yesu akawaambia viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuwa wamekuja, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba Mimi ni mnyang'anyi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Isa akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maofisa wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja mkiwa na panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyanganyi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akawaambia waliomjia, wale watambikaji wakuu na wakuu wa Patakatifu na wazee: Mmetoka wenye panga na rungu, kama watu wanavyomwendea mnyang'anyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang’anyi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akawaambia wakubwa wa makuhani, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumukamata: “Mumekuja na panga na magongo kama vile wanavyokwenda kukamata munyanganyi?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaambia waliomjia, makuhani wakuu, na majemadari wa hekalu, na wazee, Kama juu ya mnyanyangʼanyi mmetoka kwa panga na marungu?