Luke 22:56 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi mmoja wa kike alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, “Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mjakazi mmoja akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Isa!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kutokana na mwanga wa moto, mtumishi wa kike alimwona Petro amekaa pale. Akamtazama Petro usoni kwa makini. Kisha akasema, “Huyu pia alikuwa na yule mtu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mjakazi mmoja alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, “Mtu huyu alikuwa pia pamoja na Yesu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi mmoja wa kike alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, “Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtumishi mmoja wa kike, kwa kusaidiwa na mwanga wa moto, akamwona Petro ameketi pale. Akamwangalia kwa uangalifu na kusema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Yesu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtumishi mmoja wa kike akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Isa!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi akiwa katika mwanga, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi mmoja wa kike alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, “Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kijakazi alipomwona, akikaa penye mwangaza wa moto, akamkazia macho, akasema: Hata huyu alikuwa pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutumishi mumoja mwanamuke alipomwona Petro akiikaa karibu na moto, akamukazia macho na kusema: “Mutu huyu vilevile alikuwa pamoja naye.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akisema, Huyu nae alikuwa pamoja nae.